Showing posts with label NEWS. Show all posts
Showing posts with label NEWS. Show all posts

Wednesday, 26 November 2014

VYUO Tanzania vyafeli katika mjadala

Vyuo vikuu vitatu vya Tanzania ambavyo vilishiriki katika mashindano ya mjadala wa Afrika kuhusu Sheria za kimataifa za haki za kibinaadamu yalioandaliwa na kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu ICRC vimeshindwa kufika katika raundi ya mwisho.
Badala yake vyuo hivyo viliondolewa katika raundi za mapema ambapo mataifa manane ya Afrika yalishiriki.
ICRC imekuwa ikiandaa hafla kama hizo kwa kipindi cha miaka 14 sasa mjini Arusha.
Kulingana na gazeti la the Citizen nchini Tanzania, vyuo vilivyoiwakilisha Tanzania ni chuo cha kanisa katoliki cha Ruaha kutoka Iringa,Chuo cha Iringa na Chuo kikuu cha Zanzibar.
Katika raundi ya mwisho ya mashindano hayo yaliofanyika mwishoni mwa wiki katika mahakama maalum ya kimataifa inayochunguza mauaji ya kimbari nchini Rwanda ICTR mjini Arusha,chuo cha Strathmore University kutoka Kenya kiliibuka mshindi na kufuatiwa na chuo cha Christian University kutoka Uganda huku chuo cha Kunduyi pasi kutoka Zimbabwe kikiibuka mshindi wa spika bora.
Raundi ya mwisho ya mjadala huo ilisimamiwa na jaji wa mahakama hiyo Vagn Joensen,jaji wa mahakama kuu ya Tanzania Stella Mugasha,jaji wa mahakama ya haki katika Afrika mashariki Fanstin Ntezilyayo,John Joseph Wamwara na Mutsa mangezi kutoka ICRC.
Judge Joensen, ambaye alitoa zawadi kwa washindi aliyapongeza mashindano hayo kama kifaa cha kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanaofanya sheria na kwamba itasaidia kuimarisha maono yao katika siku za usoni.

Thursday, 20 November 2014

kinana awaskukia viongozi goigoi ABULRAHIMAN KINANA KATIBU MKUU WA CCM

Lindi. Viongozi wanaotokana na Chama
cha Mapinduzi (CCM),

shy-rose bhanji adaiwa kumpiga mbunge mwenzake

Dar es Salaam. Mbunge wa Bunge la Afrika
Mashariki (Eala), Shy-Rose Bhanji
ameingia katika mgogoro mpya baada ya
kutuhumiwa kumpiga mbunge mwenzake
kutoka Tanzania

Monday, 17 November 2014

kanali congo anyongwa

Mahakama ya kijeshi Mashariki mwa Jamuhuri ya
Demokrasi ya Congo imemhukumu kifo Kanali
Birocho Nzanzu baada ya kubainika na makosa ya
kutaka kumuua afisa wa jeshi la nchi hiyo
aliyekuwa mstari wa mbele kutokomeza wapiganaji
wa M23.
Kanal Mamadou Ndala anayedaiwa kuuawa na
njama za Kanal Birocho Nzanzu
Afisa anayedaiwa kupangiwa njama za kuuawa ni
Mamadou Ndala mabaye kwa kiasi kikubwa
aliamini katika vita dhidi ya kundi hilo la
wapiganaji na ambaye aliuawa mwezi januari
mwaka huu. Hata hivyo hukumu hiyo imetolewa
kwa watuhumiwa nane ambapo kati ya hao mmoja
ndiye Kanali Ndala aliyehukumiwa kifo. Mahakama
imebainisha kuwa Kanali Nzanzu amekuwa
akitumiwa na waasi wa ADF kutoka Uganda
kuandaa maujaji

Mfungwa aruhusiwa kuoa nchini marekani

Mtu aliyeua watu wengi nchini Marekani na
kufungwa kifungo cha maisha Charles Manson,
mwenye umri wa miaka 80, ameripotiwa kupewa
hati ya kuoana na mwanamke mwenye umri wa
miaka 26 ambaye amekuwa akimtembelea
gerezani.
Hati hiyo ya ndoa ilitolewa siku 10 zilizopita kwa
Manson na Afton Elaine Burton, limeripoti shirika
la habari la Associated Press.
Bi Burton alihamia Corcoran, California, miaka tisa
iliyopita ili kuwa karibu na gereza la Manson.
Manson anatumikia kifungo cha maisha jela kwa
kuua watu saba na mtoto mmoja ambaye hakuwa
amezaliwa huko Los Angeles Marekani mwaka
1969.
Waliouawa ni pamoja na mwigizaji aliyekuwa
mjamzito Sharon Tate, mke wa mwongoza sinema
Roman Polanski.
Charles Manson mfungwa mweye umri wa
miaka 80 na mke mtarajiwa Afton Elaine
Burton"Star" miaka 26
Bi Burton, ambaye anajiita nyota, ameliambia
shirika la Associated Press kuwa ataoana na
Manson mwezi ujao. Hati hiyo imeripotiwa
kudumu kwa siku 90.
"Wote mtajua kuwa ni kweli... Itatokea,"
ameliambia shirika hilo.
"Nampenda," ameongeza kusema.
Kiongozi huyo wa kidini na wafuasi wake,
wakijulikana kama Familia ya Manson, aliwachoma
visu na kuwaua kwa kuwapiga risasi watu saba
huko Los Angeles katika siku mbilimwezi Agosti
1969 katika jaribio la kutaka kuanza vita vipya vya
matabaka ya rangi.
Manson na wanawake watatu washirika wake
walihukumiwa adhabu ya kifo kutokana na mauaji
hayo, lakini hukumu hiyo ilitolewa mwaka 1972
wakati jimbo la California lilipositisha kwa muda
adhabu ya kifo.
Mwaka 2012, Manson alinyimwa parole yaani
msamaha wa kuachiliwa na jopo la gereza la
California - ilikuwa mara ya 12 kwa Manson
kuomba kuachiliwa huru.
Kwa matokeo hayo, Manson hastahili tena kuomba
parole hadi mwaka 2027.
Mshirikish

familia ya kassig yamlilia abdul-rahman

Wazazi wa Abdul-Rahman Kassig raia wa Marekani
aliyekuwa akifanya kazi katika mashirika ya
misaada ya kibinadamu nchini Syria ,wametoa
rambi rambi zao kwa mtoto wao aliyeuawa kwa
kuchinjwa na wapiganaji wa IS.
Wamesema kuwa wamejifunza kutokana na maujaji
hayo na kwamba wamewasamehe wauaji hao japo
kuwa awali mioyo yao ilikuwa na huzuni mkubwa
na uchungu kufuatia tukio hilo.
Ed na Paula Kassig wadogo zake na Abdul
Rahman Kassig wamemuelezea ndugu yao
kwamba alikuwa mkweli na mfanyakazi mwaminifu
katika mashirika ya kutoa misaada ya kibidamu
ambaye alikuwa na mtazamo wa kutoa msaada na
kujiepusha na udanganyifu wa aina yoyote.
Hata hivyo familia hiyo ya Kassig imetoa rai ya
kufanyika kwa maombi maalumu kwa watu wa
Syria nchini Iraq na duniani kote mahala ambapo
watu wanakabiliwa na vitendo vya ukiukwaji wa
haki.
Awali waziri wa kigeni wa Ufaransa Bernard
Cazeneuve amesema kuna uwezekano mkubwa
raia wa nchi hiyo walishiriki katika kitendo cha
kumchinja Abdul kutokana na picha za video
zilizoonyeshwa jumapili ambapo anaonekana
Kassig na wanajeshi wengine 18 wa Syria.

AKANA NJAMA KUMUUA MUGABE

Makamu wa Rais nchini Zimbabwe, anasema
anapanga kuchukua hatua za kisheria dhidi ya
shirika la habari la kitaifa kwa kumhusisha na
njama ya kumuua Rais Robert Mugabe.
Joyce Mujuru amesema amewaamuru mawakili
wake kumrejeshea hadhi yake ya kisiasa baada ya
kuhusishwa na madai hayo ya uhaini pamoja na
ufisadi.
Jarida la Sunday Mail la nchini humo, limeripoti
kuwa kuna njama ya kumkodi mamluki kumuua
Mugabe ili Bi Mujuru achukue mamlaka.
Mwezi jana Bwana Mugabe alifikisha miaka 90 na
kusema hana nia ya kuachia madaraka.
Ametawala Zimbabwe tangu nchi hio kujipatia
uhuru mwaka 1980.
'Ushetani'
Rais Mugabe akiwa na mkewe Grace Mugabe
Rais Mugabe na Bi Mujuru walikuwa wandani wa
karibui lakini kwa sasa wamehasimiana huku
mjadala wa kumrithi Mugabe ukitokota katika
chama tawala cha Zanu-PF kikijiandaa kwa
kongamano lake la kitaifa mwezi ujao.
Mkewe Bwana Mugabe, Grace Mugabe amekuwa
akiendesha kampeini dhidi ya Bi Mujuru akimtaka
astaafu.
Amemtuhumu Bi Mujuru kwa kuwa mtu wa
kishetani na mwenye kugawanya watu pamoja na
kujipatia pesa kwa njia ya udanganiyifu, kutoka
kwa makampuni.
Taarifa ya bi Mujuru akikana madai ya njama hiyo
haikutarajiwa.
Ingawa hajaonyesha dalili za kuachia ngazi,
anakabiliwa na shinikizo kali sana za kisiasa.
Jarida la Sunday mail liliripoti taarifa hizo za
kushtua kwamba bi Mujuru na washirika wake
wanapanga kumkodi mamluki ambaye atamuua
Mugabe ili achukue mamlaka.
"ninakanusha madai hayo ya uhaini na ufisadi
pamoja na kutumia vibaya mamlaka yangu, madai
ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi yangu kwa
mda mrefu sasa,'' alisema Mujuru.
Amewataka mawakili wake kuchukua hatua za
haraka za kisheria dhidi ya waliotoa madai hayo
na kumharibia sifa yake.

DAKTARI MAREKANI AFA KWA EBOLA

Daktari Martin Salia kutoka nchini Sierra Leone
aliyekuwa anapokea matibabu ya Ebola nchini
Marekani amefariki.

Friday, 19 September 2014

KAMANDA MWANAMKE KUKAMATWA

Kamanda mwanamke muasi
akamatwa
19 Septemba 2014 Imebadilishwa mwisho saa
13:26 GMT
Mshirikishe mwenzako
Waasi wa CharlesTaylor walikuwa wakiwatumia
watoto kama wapiganaji
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameisifu
hatua ya kukamatwa nchini Ubelgiji kwa kamanda
mwanamke aliyekuwa katika kikundi cha waasi cha
Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor.
Kamanda huyo amekamatwa kwa makosa ya jinai
aliyoyafanya wakati wa vita vya wenyewe kwa
wenyewe nchini Liberia.
Hatua ya kukamatwa kwa kamanda huyo, imekuja
baada ya malalamiko kuwasilishwa kwa niaba ya
waathiriwa watatu wa vita hivyo, mwaka 1992.
Martina Johnson, bado hajatoa jibu lolote kwa
madai yaliyowasilishwa mahakamani dhidi yake
yakiwemo kuwaua watu kinyama na kuwakatakata
vipande
Taylor amefungwa jela baada ya kupatikana na
hatia ya uhalifu wa kivita nchini Siera Leone.
Mahakama maalum ya Umoja wa Mataifa ilimpata
na hatia Taylor mwaka 2012 kwa kosa la
kusambaza silaha kwa waasi nchini Siera Leone
huku naye akipewa madini ya Almasi na waasi
hao.
Alianzisha uasi nchini Liberia mwaka 1989 na
hatimaye kuwa Rais mwaka 1997 lakini
akalazimika kukimbia nchi hiyo baada ya kundi
lengine la waasi kuanzisha uasi mwaka 2003.
Shirika moja mjini Geneva, ambalo lilisaidia
kufikisha kesi dhidi ya Bi Johnson mahakamani,
limesema kwamba tangu kumalizika kwa vita vya
wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia mwaka
2003, hakuna juhudi zozote zimefanywa
kuchunguza na kufikisha mahakamani kesi za
uhalifu uliotendwa wakati wa vita nchini Liberia.
Hii ni licha ya mapendekezo yaliyotolewa mwaka
2009 na tume ya ukweli na maridhiano ya Liberia.