Lindi. Viongozi wanaotokana na Chama
cha Mapinduzi (CCM),
wametakiwacha Mapinduzi (CCM),
kushughulikia matatizo ya wananchi
badala ya kuunda kamati kwa ajili ya
kufuatilia makosa yanayofanywa na
baadhi ya watendaji.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana alitoa agizo hilo jana
alipozungumza na wakazi wa Jimbo la
Mtama.
Kinana alisema wananchi wanahitaji
maendeleo yatakayotokana na usimamizi
na utendaji bora wa viongozi wanaotoka
CCM.
“Kiongozi bora ni yule anayechukua
uamuzi kiutendaji na si yule anayefumbia
macho makosa na kazi yake inakuwa ni
kuunda kamati wakati wananchi
wanachohitaji ni huduma,” alisema
Kinana.
Kinana pia alisema CCM inasikitishwa na
wanunuzi wa korosho wanaopanga bei ili
kumuumiza mkulima.
Alisema Lindi na Mtwara ni mikoa
inayozalisha korosho kwa wingi, lakini
cha kushangaza hawana viwanda.
Kinana alisema waliopewa dhamana ya
kufufua viwanda hivyo nao
wameshindwa, badala yake wamevigeuza
maghala ya kuhifadhia korosho na
kwenda kuuza nje ya nchi kwa bei ghali,
ilhali mkulima akiendelea kuteseka.
No comments:
Post a Comment