Thursday, 20 November 2014

UKAWA NA NJAMA ZA IPTL

Dodoma. Wakati kamati ya Bunge ya
Hesabu za Serikali (PAC) ikianza kupitia
ripoti ya IPTL kuhusu uchunguzi wa
ufisadi katika Akaunti ya Tegeta Escrow,

wabunge wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), umedai kwamba kuna
mikakati imeandaliwa kuzima ripoti hiyo
kusomwa na kujadiliwa bungeni.
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James
Mbatia alisema jana kwamba moja ya
mikakati hiyo ni madai ya kuwapo barua
ya Mahakama kuzuia mjadala huo
akisema mkakati huo unatokana na
ukubwa wa kashfa na jinsi
inavyowahusisha viongozi waandamizi
serikalini.
Mbatia aliyeambatana na kundi kubwa la
wabunge kutoka Chadema, CUF na NCCR-
Mageuzi, alisema: “Iko mikakati na mbinu
za kila aina kulihujumu Bunge
lisisimamie fedha za walipakodi, ndiyo
maana kuna danadana na tuna taarifa za
kuwapo barua kutoka mahakamani
kuzuia jambo hilo lisijadiliwe bungeni
kwa madai eti kuna kesi.
“Mahakama haiwezi kuingilia shughuli za
Bunge, inatia wasiwasi kwa kuwa Ofisi ya
Bunge nayo imekuwa na danadana kila
siku kwa kubadilisha badilisha ratiba
wakati sisi tunataka hawa waliohusika
kwenye kashfa hii wachukuliwe hatua.”
Pia, alisema kuna taarifa kwamba Serikali
inadai haina fedha, ikitaka kufupisha
Bunge na suala hilo lisijadiliwe sasa hivi.
Mbunge wa Mkanyageni (CUF),
Mohammed Mnyaa alisema: “Serikali
inategesha tegesha tu mambo bungeni na
ndiyo maana leo (jana) wameahirisha
Bunge hadi kesho (leo) bila sababu za
msingi, wanafinya muda wa sisi kujadili
sakata hili,” alisema Mnyaa.
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani,
Tundu Lissu alisema escrow ni kama
ilivyokuwa kashfa ya Richmond ambayo
iliwang’oa wahusika wakuu bungeni,
hivyo haiwezekani isijadiliwe bungeni
kwa madai kwamba Mahakama imezuia...
“Hakuna utaratibu kama huo wa
Mahakama kuelekeza Bunge kitu gani
kifanyike na gani kisifanyike pia hata
Katiba hairuhusu hilo.”
Lissu alishangazwa na Naibu Spika, Job
Ndugai kuahirisha Bunge jana hadi leo
kwa madai kuwa yeye (Lissu) alikuwa
hajakamilisha taarifa ya upinzani kwenye
muswada wa Sheria ya Marekebisho ya
Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2014 akidai
kuwa huo ni upotezaji wa muda.
“Nilimwomba Naibu Spika kuwa
aahirishe muswada huo hadi kesho kwa
kuwa ulikuwa umepangwa tarehe 25
lakini ghafla ukabadilishwa na mimi
sikuwapo kwa muda wote huo. Sikuomba
aahirishe Bunge nilimwomba aahirishe
muswada tu,” alisema Lissu.
ADVERTISEMENT
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alisema
naye amesikia kuwapo barua ya
Mahakama kuzuia mjadala huo na
kusema kama ni kweli, halitakuwa sahihi.
Akizungumza kwenye mkutano wa
hadhara katika Operesheni Delete CCM
mjini Dodoma jana, Katibu Mkuu wa
Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema si
Waziri Mkuu wala Jaji Mkuu anayeweza
kuuzima mjadala wa escrow bungeni.
Alisema kashfa hiyo ambayo chama chake
kina nyaraka zake na ripoti za uchunguzi
wa escrow na Takukuru, lilianzia bungeni
na lazima lijadiliwe na kumalizikia
bungeni.
Ndugai ajibu hoja
Akizungumzia madai hayo, Ndugai
alisema hajui kama kuna barua kutoka
mahakamani kuzuia mjadala wa escrow
bungeni na suala hilo litawasilishwa na
PAC bungeni Novemba 27 kama
ilivyopangwa.
“Waiamini kamati, kwanza hawa wa
upinzani ni yao (kamati) haiongozwi na
CCM, mimi naamini kamati itafanya kazi
nzuri. Sidhani kama kanuni zinaruhusu
kugawa ripoti hiyo kwa kuwa ni siri,
kanuni hairuhusu.”
Rejea
Ripoti ya Tegeta Escrow inatokana na
uchunguzi maalumu wa Sh306 milioni
zilizochotwa katika akaunti ya escrow
ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Fedha hizo zilitokana na gharama za
uwekezaji zilizokuwa zinalipwa na
Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL baada
ya kutokea mgogoro wa kibiashara baina
ya wabia hao.
Tanesco ililalamika kuwa ilikuwa inailipa
zaidi IPTL kinyume na gharama halisi za
uwekezaji, hivyo kuamuliwa na
Mahakama kuwa fedha hizo ziwekwe
katika escrow hadi upatikane ufumbuzi
wa mgogoro huo lakini zikachukuliwa
kabla kesi kuamuliwa.H

No comments:

Post a Comment