Wazazi wa Abdul-Rahman Kassig raia wa Marekani
aliyekuwa akifanya kazi katika mashirika ya
misaada ya kibinadamu nchini Syria ,wametoa
rambi rambi zao kwa mtoto wao aliyeuawa kwa
kuchinjwa na wapiganaji wa IS.
Wamesema kuwa wamejifunza kutokana na maujaji
hayo na kwamba wamewasamehe wauaji hao japo
kuwa awali mioyo yao ilikuwa na huzuni mkubwa
na uchungu kufuatia tukio hilo.
Ed na Paula Kassig wadogo zake na Abdul
Rahman Kassig wamemuelezea ndugu yao
kwamba alikuwa mkweli na mfanyakazi mwaminifu
katika mashirika ya kutoa misaada ya kibidamu
ambaye alikuwa na mtazamo wa kutoa msaada na
kujiepusha na udanganyifu wa aina yoyote.
Hata hivyo familia hiyo ya Kassig imetoa rai ya
kufanyika kwa maombi maalumu kwa watu wa
Syria nchini Iraq na duniani kote mahala ambapo
watu wanakabiliwa na vitendo vya ukiukwaji wa
haki.
Awali waziri wa kigeni wa Ufaransa Bernard
Cazeneuve amesema kuna uwezekano mkubwa
raia wa nchi hiyo walishiriki katika kitendo cha
kumchinja Abdul kutokana na picha za video
zilizoonyeshwa jumapili ambapo anaonekana
Kassig na wanajeshi wengine 18 wa Syria.
Monday, 17 November 2014
familia ya kassig yamlilia abdul-rahman
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment