Monday, 17 November 2014

Mfungwa aruhusiwa kuoa nchini marekani

Mtu aliyeua watu wengi nchini Marekani na
kufungwa kifungo cha maisha Charles Manson,
mwenye umri wa miaka 80, ameripotiwa kupewa
hati ya kuoana na mwanamke mwenye umri wa
miaka 26 ambaye amekuwa akimtembelea
gerezani.
Hati hiyo ya ndoa ilitolewa siku 10 zilizopita kwa
Manson na Afton Elaine Burton, limeripoti shirika
la habari la Associated Press.
Bi Burton alihamia Corcoran, California, miaka tisa
iliyopita ili kuwa karibu na gereza la Manson.
Manson anatumikia kifungo cha maisha jela kwa
kuua watu saba na mtoto mmoja ambaye hakuwa
amezaliwa huko Los Angeles Marekani mwaka
1969.
Waliouawa ni pamoja na mwigizaji aliyekuwa
mjamzito Sharon Tate, mke wa mwongoza sinema
Roman Polanski.
Charles Manson mfungwa mweye umri wa
miaka 80 na mke mtarajiwa Afton Elaine
Burton"Star" miaka 26
Bi Burton, ambaye anajiita nyota, ameliambia
shirika la Associated Press kuwa ataoana na
Manson mwezi ujao. Hati hiyo imeripotiwa
kudumu kwa siku 90.
"Wote mtajua kuwa ni kweli... Itatokea,"
ameliambia shirika hilo.
"Nampenda," ameongeza kusema.
Kiongozi huyo wa kidini na wafuasi wake,
wakijulikana kama Familia ya Manson, aliwachoma
visu na kuwaua kwa kuwapiga risasi watu saba
huko Los Angeles katika siku mbilimwezi Agosti
1969 katika jaribio la kutaka kuanza vita vipya vya
matabaka ya rangi.
Manson na wanawake watatu washirika wake
walihukumiwa adhabu ya kifo kutokana na mauaji
hayo, lakini hukumu hiyo ilitolewa mwaka 1972
wakati jimbo la California lilipositisha kwa muda
adhabu ya kifo.
Mwaka 2012, Manson alinyimwa parole yaani
msamaha wa kuachiliwa na jopo la gereza la
California - ilikuwa mara ya 12 kwa Manson
kuomba kuachiliwa huru.
Kwa matokeo hayo, Manson hastahili tena kuomba
parole hadi mwaka 2027.
Mshirikish

No comments:

Post a Comment