Kamanda mwanamke muasi
akamatwa
19 Septemba 2014 Imebadilishwa mwisho saa
13:26 GMT
Mshirikishe mwenzako
Waasi wa CharlesTaylor walikuwa wakiwatumia
watoto kama wapiganaji
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameisifu
hatua ya kukamatwa nchini Ubelgiji kwa kamanda
mwanamke aliyekuwa katika kikundi cha waasi cha
Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor.
Kamanda huyo amekamatwa kwa makosa ya jinai
aliyoyafanya wakati wa vita vya wenyewe kwa
wenyewe nchini Liberia.
Hatua ya kukamatwa kwa kamanda huyo, imekuja
baada ya malalamiko kuwasilishwa kwa niaba ya
waathiriwa watatu wa vita hivyo, mwaka 1992.
Martina Johnson, bado hajatoa jibu lolote kwa
madai yaliyowasilishwa mahakamani dhidi yake
yakiwemo kuwaua watu kinyama na kuwakatakata
vipande
Taylor amefungwa jela baada ya kupatikana na
hatia ya uhalifu wa kivita nchini Siera Leone.
Mahakama maalum ya Umoja wa Mataifa ilimpata
na hatia Taylor mwaka 2012 kwa kosa la
kusambaza silaha kwa waasi nchini Siera Leone
huku naye akipewa madini ya Almasi na waasi
hao.
Alianzisha uasi nchini Liberia mwaka 1989 na
hatimaye kuwa Rais mwaka 1997 lakini
akalazimika kukimbia nchi hiyo baada ya kundi
lengine la waasi kuanzisha uasi mwaka 2003.
Shirika moja mjini Geneva, ambalo lilisaidia
kufikisha kesi dhidi ya Bi Johnson mahakamani,
limesema kwamba tangu kumalizika kwa vita vya
wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia mwaka
2003, hakuna juhudi zozote zimefanywa
kuchunguza na kufikisha mahakamani kesi za
uhalifu uliotendwa wakati wa vita nchini Liberia.
Hii ni licha ya mapendekezo yaliyotolewa mwaka
2009 na tume ya ukweli na maridhiano ya Liberia.
Friday, 19 September 2014
KAMANDA MWANAMKE KUKAMATWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment