Makamu wa Rais nchini Zimbabwe, anasema
anapanga kuchukua hatua za kisheria dhidi ya
shirika la habari la kitaifa kwa kumhusisha na
njama ya kumuua Rais Robert Mugabe.
Joyce Mujuru amesema amewaamuru mawakili
wake kumrejeshea hadhi yake ya kisiasa baada ya
kuhusishwa na madai hayo ya uhaini pamoja na
ufisadi.
Jarida la Sunday Mail la nchini humo, limeripoti
kuwa kuna njama ya kumkodi mamluki kumuua
Mugabe ili Bi Mujuru achukue mamlaka.
Mwezi jana Bwana Mugabe alifikisha miaka 90 na
kusema hana nia ya kuachia madaraka.
Ametawala Zimbabwe tangu nchi hio kujipatia
uhuru mwaka 1980.
'Ushetani'
Rais Mugabe akiwa na mkewe Grace Mugabe
Rais Mugabe na Bi Mujuru walikuwa wandani wa
karibui lakini kwa sasa wamehasimiana huku
mjadala wa kumrithi Mugabe ukitokota katika
chama tawala cha Zanu-PF kikijiandaa kwa
kongamano lake la kitaifa mwezi ujao.
Mkewe Bwana Mugabe, Grace Mugabe amekuwa
akiendesha kampeini dhidi ya Bi Mujuru akimtaka
astaafu.
Amemtuhumu Bi Mujuru kwa kuwa mtu wa
kishetani na mwenye kugawanya watu pamoja na
kujipatia pesa kwa njia ya udanganiyifu, kutoka
kwa makampuni.
Taarifa ya bi Mujuru akikana madai ya njama hiyo
haikutarajiwa.
Ingawa hajaonyesha dalili za kuachia ngazi,
anakabiliwa na shinikizo kali sana za kisiasa.
Jarida la Sunday mail liliripoti taarifa hizo za
kushtua kwamba bi Mujuru na washirika wake
wanapanga kumkodi mamluki ambaye atamuua
Mugabe ili achukue mamlaka.
"ninakanusha madai hayo ya uhaini na ufisadi
pamoja na kutumia vibaya mamlaka yangu, madai
ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi yangu kwa
mda mrefu sasa,'' alisema Mujuru.
Amewataka mawakili wake kuchukua hatua za
haraka za kisheria dhidi ya waliotoa madai hayo
na kumharibia sifa yake.
Monday, 17 November 2014
AKANA NJAMA KUMUUA MUGABE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment