UJASIRIAMALI: Mitaji midogo
kikwazo kwa vikundi
>Ukosefu wa mbinu za kuboresha bidhaa, mtaji
mdogo, matatizo ya afya na ukosefu wa mbinu za
kikwazo kwa vikundi
>Ukosefu wa mbinu za kuboresha bidhaa, mtaji
mdogo, matatizo ya afya na ukosefu wa mbinu za
ADVERTISEMENT
Dar es Salaam. Ukosefu wa mbinu za
kuboresha bidhaa, mtaji mdogo, matatizo
ya afya na ukosefu wa mbinu za
kuendeleza mikopo midogo ni miongoni
mwa matatizo yanayowakabili wanawake
waliojiajiri katika shughuli za usindikaji
vyakula na utengenezaji wa bidhaa za
mikono.
Hayo yalibainishwa na wanawake
wajasiriamali kutoka kikundi cha
Vimosewa nchini India ambao wako
nchini kwa warsha ya siku mbili kwa ajili
ya kubadilishana uzoefu na wanawake
wajisiriamali wa Dar es Salaam.
Akizungumzia uzoefu katika sekta ya
ujasiriamali kutoka India, Mirai
Chatterjee, ambaye ni mwenyekiti wa
Vimosewa, alisema wanawake wengi
waliojiajiri wanashidwa kuendelea
kutokana na kukosa ujuzi wa namna ya
kuongeza thamani kwa bidhaa
wanazozalisha ili kuvutia soko kubwa
zaidi.
Alisema changamoto ya mitaji pia
huwakabili wajasiriamali wengi, hivyo
kuwataka wale wa nchini kuanzisha
vyama vyao vya kuweka na kukopa,
jambo litakalowawezesha kujiongezea
mtaji kwa kulipa riba nafuu.
“Tumeanza harakati hizi za kujikomboa
kiuchumi, takribani miaka 30 iliyopita.
Pamoja na ukongwe tuliokuwa nao, bado
tuna changamoto ndogondogo
zinazotukabili,” alisema.
Said Wamba, katibu mkuu wa Chama
chama cha Wafanyakazi wa Hifadhi,
Mahoteli, Majumbani, Huduma za Jamii
na Ushauri (Chodawu) ambao ni
waandaaji wenza wa warsha hiyo,
alisema suala la uangalizi wa afya kwa
wanawake waliojiajiri pia limekuwa
changamoto katika maendeleo ya kazi
zao. Alisema kuwa katika shughuli zao,
wengi husahahu suala la kulinda afya zao
na matokeo yake, huathirika na kemikali
wanazotumia kutengeneza bidhaa, hivyo
kushindwa kutimiza ndoto zao za
mafanikio.
No comments:
Post a Comment