Wednesday, 12 November 2014

Rapa Geez mabovu afariki dunia usiku huu

Rapper aliekuwa anawakilisha Dirty South,  Ahmed Ally Upete, a.k.a "Geez Mabovu" amefariki dunia jioni ya leo (November 11)  mishale ya sa moja akiwa kwao mkoani iringa

Geez ameugua kwa muda mrefu na baada ya hali yake kuonekana sio nzuri kaka yake alikuja kumchukua na kurudi nae mkoani Iringa, ameniambia mdogo wake ambae pia ni msanii  "Mad P" kupitia ujumbe mfupi wa maneno. habari zaidi utaendelea kuzipata kila zinapotufikia

Mabovu alikuja juu sana baada ya kutoa ngoma inayoitwa  Mtoto Wa Kiume na dakika sifuri aliyomshirikisha marehem Albert Mangwea

No comments:

Post a Comment