Wednesday, 12 November 2014

Mtoto wa beckham asaini mkata klabu kubwa duniani

Mtoto wa kwanza wa mchezaji wa zamani wa Manchester United  Beckham na mwanamitindo Victoria amesign kuichezea timu ya mpira wa miguu "Arsenal"

Brookyln (15)aliyewahi kufanya mazoezi na klabu hiyo ya London amekataa kufuata nyayo za mzazi wake na kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu hiyo licha ya fuatiliwa kwa karibu na klabu kama Chelsea na  Manchester United.
Gazeti la The Daily Star lilifichua kuwa Brooklyn amesaini mkataba wa awali wa mwaka mmoja baada ya kuwafurahisha makocha wa klabu hiyo wakati wa mazoezi aliyofanya klabuni hapo hivi karibuni.

Inadaiwa kwamba Arsenal wamekuwa wakimfuatilia chipukizi huyo kwa muda mrefu na wapo tayari kumpa mkataba wa muda mrefu, endapo ataendelea kung’ara msimu huu.
Chanzo cha habari kilichonukuliwa na The Daily Star kimefichua kuwa Brooklyn ni kijana mwenye kipaji kikubwa , ameonyesha ukomavu na utulivu kwenye mazoezi, hata mechi za timu ya watoto ambazo amekuwa akichezeshwa.
Watoto wa Beckham wamekuwa sehem ya Arsenal kwa miaka sasa huku Romeo mwenye miaka 12 kwa sasa anachezea arsenal kwa wenye umri chini ya miaka 13, na Cruz (9) anachezea team ya wenye miaka chini ya miaka 10, club iko London na Beckham ni rafiki wa manager wa Arsenal, Arsene Wenger.

No comments:

Post a Comment