Kocha mkuu wa klabu ya Mbeya City Juma
Mwambuzi ameamua kutundika daruga
katika timu hiyo kufuatia matokeo pamoja na
mawasiliano mabovu na uongozi.
Akizungumza na mwandishi wetu kocha
huyo bora wa ligi kuu msimu wa mwaka jana
ambaye aliipandisha daraja Mbeya City na
kuleta upinzani mkubwa kwa timu za Simba,
Yanga na Azam amesema ameamua
kuwaachia viongozi timu yao ili watafute
kocha atakaefaa.
Mwambusi ameelezea sababu ya kubwaga
manyanga kuwa kuwepo kwa tuhuma za
kiufundi baada ya timu hiyo kuwa na
matokeo mabovu msimu huu kitu ambacho
kinahusishwa na familia yake, lakini hakuwa
tayari kuzungumza kwa kina nini tuhuma
hizo.
“Ni kweli nimeamua kuondo na kesho ndio
nitapeleka barua yangu katika uongozi,
Kikubwa nimeona niwapishe viongozi baada
ya kuwepo na mtafaruku mkubwa tu kitu
ambacho matatizo ya timu wanayahusisha
na familia yangu kisha nimeoa mwanamke
wa Zanzibar” Amesema Mwambusi ambaye
mwakana amemaliza mzunguko wa kwanza
bila kufungwa.
Hadi sasa Mwambusi anabwaga manyanga
Mbeya City ikiwa inashika mkia wa ligi kuu
baada ya kucheza michezo saba kufungwa
minne, kushinda mchezo mmoja na kutoa
sare miwili ikiwa imevuna pointi 5.
Uongozi wa klabu hiyo ulipoulizwa na
amwandisjhi wetu kupitia kwa Dismas Ten
afisa habari wa klabu hiyo amesema kuwa
wao hawana taarifa za kuondoka kwa kocha
huyo huku akisisitiza kuwa bado ni kocha
wao.
Monday, 17 November 2014
KOCHA MWAMBUSI ABWAGA MANYANGA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment